Web Analytics
Biolojia - Wikipedia

Biolojia

Kutoka Wikipedia

Biolojia ni elimu ya uhai na viumbehai kama vile mimea, wanyama, kuvu (kama uyoga), bakteria na virusi.

Biolojia inaangalia jinsi viumbehai vinavyoishi na jinsi vinavyohusiana kati yao na katika mazingira yao. Lugha ya kisayansi katika biolojia inatumia maneno mengi ya asili ya Kigiriki na Kilatini. Lugha nyingi zimeingiza maneno haya tu katika msamiati wao; katika lugha kadhaa wataalamu wametafsiri sehemu ya maneno haya kwa lugha zao lakini kwa ujumla sehemu kubwa na majina ya kisayansi hufuata utaratibu wa Kigiriki na Kilatini.

Kama sayansi baiolojia ina matawi au masomo mengi. Kuna njia mbalimbali kuyataja, mmojawapo ni:

  • zoolojia : somo kuhusu wanyama
  • botania : somo kuhusu mimea
  • mikrobiolojia : somo kuhusu bakteria na viumbehai vidogo sana

Wataalamu wengi huona ya kwamba viumbehai vyote hugawiwa katika sehemu au milki kubwa tatu:

o Protista viumbe vyenye chembe kimoja to
o Fungi au kuvu (kama vile uyoga)
o Animalia au wanayama
o Planta au mimea

Kati ya masomo madogo mengi ndani ya biolojia kuna yafuatayo:

  • Anatomia na Morpholojia - zinaangalia jinsi viumbehai vinavyoonekana na muundo wa miili yao
  • Taxonomia au uainishaji - inaangalia jinsi ya kugawa viumbehai katika vikundi na kuvipa majina ya kisayansi
  • Ekolojia - inaangalia uhusiano wa viumbehai na mazingira yao, pamoja na athari ya mabadiliko ya mazingira
  • Etholojia -inaangalia mwenendo na mazoea ya viumbehai
  • Fiziolojia - inaangalia jinsi viumbehai vinaishi, vinavyokula au kujilisha
  • Biokemia - inaangalia kemia ndani ya viumbehai
  • Paleontolojia - inaangalia spishi zilizokwisha tangu miaka mingi ikionekana katika mawe, kwa mfano madinosauri
Lugha nyingine